1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tishio la kigaidi Ujerumani

18 Novemba 2010

Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas De Maiziere aonya kuhusu tishio la kigaidi nchini.

https://p.dw.com/p/QCE4
Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere.Picha: picture-alliance/dpa

Waziri wa ndani wa Ujerumani Thomas De Maiziere ameonya kwamba maafisa wa usalama wana ushahidi mpya na wa kuaminika kwamba wanamgambo wa kiislamu  wanapanga shambulio la kigaidi  nchini Ujerumani kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri Maiziere amewaambia waandishi wa habari katika mkutano nao uliofanyika mjini Berlin hapo jana, kwamba kutokana na hilo, anazidisha kiwango cha tahadhari kwa shambulio la kigaidi.

De Maiziere amesema ameamrisha kuzidishwa marudufu uwepo wa maafisa wa polisi wanao onekana na wa siri nchini. Amesema taarifa hizo zimepokewa kutoka Yemen na amewaomba raia kuwa waangalifu.

Razzia Islam München
Maafisa wa polisi nchini Ujerumani.Picha: AP

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimezinukuu duru za usalama vikisema kwamba  hadi magaidi wanne wenye itikadi kali za dini ya kiislamu wanaelekea Ujerumani kutekeleza mashambulio.

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/DPAE