1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo: Japan itaacha kuvua nyangumu katika eneo la Antarctic mnamo msimu huu

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNl

Japan imeacha kuvuwa nyangumi katika eneo la Antarctic mnamo msimu huu, baada ya meli yake kubwa ya kuvuwa nyangumi kukumbwa na moto wiki mbili zilizopita. Meli ya Japan ya Nisshin Maru, ilio na uzito wa tani alfu nane, injini yake ilianza tena kufanya kazi mwisho wa wiki iliopita baada ya kukwama katika bahari iliojaa barafu tangu moto huo kuzuka na ambao ulimuuwa baharia mmoja. Wakala wa uvuvi wa Japan ulisema meli hiyo iliweza kusafiri yenyewe kwa nguvu ya injini yake, lakini kutokana na uharibifu wa vifaa ndani ya meli hiyo kwa sababu ya moto uliotokea, itakuwa shida kuendelea na uvuvi. Zoezi hilo la uvuvi lilizusha sokomoko wiki iliopita pale walinzi wa mazingira walipoishambulia meli hiyo kwa mabomu ya moshi.