1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Kimbunga chasababisha maafa nchini Japan

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCv9

Kimbunga kimepiga kwenye eneo moja la kaskazini mwa Japan na kusababisha mauaji ya watu 9 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Shirika la habari la Kyodo, limesema kwa uchache watu 20 wameangukiwa na nyumba zilizojengwa karibu na sehemu kunakojengwa njia ya leri ya chini ya ardhi katika mji wa Saroma katika kisiwa cha Hokkaido kaskazini mwa nchi hiyo.

Waokozi walikuwa wakijaribu kuwaokoa watu walionasa katika vifusi vya nyumba zilizoporomoka lakini watu wanne hadi sasa hawajapatikana.