1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Wasiwasi wapungua kuhusu kutokea kimbunga cha Tsunami nchini Japan

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCat

Wasiwasi uliokuwepo wa kimbunga cha Tsunami kupiga pwani ya kaskazini mashariki mwa Japan, umepungua baada ya mawimbi madogo kupiga eneo hilo la pwani ya bahari ya Pasifik iliyokuwa imekumbwa na tetemeko kubwa.

Maelfu ya wakazi walikuwa wamekimbilia katika nyanda za juu ingawa mawimbi hayo yaliyopiga katika kisiwa cha Hokkaido hayakuwa makubwa.

Maafisa wa serikali ya Marekani pia wameondoa tahadhari waliokuwa wametangaza katika majimbo ya Alaska na Hawaii baada ya kuhakikisha kwamba mawimbi yaliyopiga hayakuwa hatari.

Tetemeko hilo lililokuwa na uzito wa nane nukta tatu katika vipimo vya Richter, lilianzia mashariki mwa visiwa vya Kuril.