1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Waziri Mkuu Shinzo Abe amejiuzulu

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQV

Waziri Mkuu wa Japani,Shinzo Abe amejiuzulu. Alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Tokyo alisema,raia wanahitaji kiongozi mpya wanaomuamini.Abe alieshika madaraka mwaka mmoja uliopita,amepoteza imani ya umma kwa sababu ya kashfa mbali mbali zilizotokea ikiwa ni pamoja na uongozi mbaya kuhusika na mfumo wa malipo ya uzeeni.

Katika uchaguzi wa bunge kuu uliofanywa mwezi wa Julai,chama chake cha KiLiberal kilipoteza wingi wake bungeni.Vile vile,juhudi zake za kutaka kurefusha ujumbe wa Japan nchini Afghanistan zinapingwa vikali bungeni.Abe alikwisha onya kuwa atajiuzulu,pindi upinzani utazuia kuidhinisha kurefusha ujumbe wa nchini Afghanistan.