1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Chama cha LDP kumchagua kinara wake

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNT

Chama kinachotawala nchini Japan cha Liberal Democratic Party kinajiandaa kumchagua kiongozi wake mpya katika kura ambayo inatarajiwa kuamua ni nani atakae chukuwa mahala pa aliyekuwa waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Watetezi wawili katika wadhfa huo ni waziri wa zamani wa mambo ya nje Taro Aso na katibu wa zamani wa baraza la mawaziri Yasuo Fukuda ambae anatarajiwa zaidi kuchukuwa nafasi hiyo ya waziri mkuu wa Japan.

Bwana Shinzo Abe alijiuzulu kwa ghafla wiki mbili zilizopita kufuatia kashfa kadhaa za kisiasa na kushindwa vibaya chama chake katika uchaguzi uliomalizika wa mwezi Julai.