1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Idadi ya watu waliokufa yaongezeka

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBi3

Idadi ya awatu waliokufa kufuatia tetemeko la ardhi kaskazini magharibi mwa Japan imeongezeka na kufikia watu sita, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia tetemeko hilo la kiwango cha rishta 6.8 ambalo lilituwama katika wilaya ya Naiigata kilomita 250 kaskazini mwa mji mkuu wa Tokyo.

Tetemeko hilo pia lilisababisha moto katika mtambo wa umeme kwenye kiwanda cha nguvu za nyuklia. Maafisa kwenye kiwanda hicho wamefahamisha kwamba walifanikiwa kudhibiti usalama kwa kukifunga kiwanda hicho mara moja.

Mitetemeko mingine imeripotiwa kutokea baada ya tetemeko la kwanza ikiwa ni pamoja na tetemeko la kiwango cha rishta 5.6.