1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO:Marekani yaridhia mwelekeo wa mashauriano kuhusu mradi wa Korea Kaskazini wa silaha za kinyuklia.

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZS

Mjumbe wa Marekani wa Korea Kaskazini, Christopher Hill, amesema ana matumaini makubwa ya kufanikiwa mashauriano yanayoitaka Korea Kaskazini kusitisha mradi wake wa silaha za kinyuklia.

Christopher Hill alikuwa akizungumza mjini Tokyo, Japan katika kituo chake cha pili cha ziara ya mataifa ya Eshia.

Mjumbe huyo wa Marekani alisema mashauriano ya hivi karibuni mjini Berlin yaliweka msingi mzuri wa mkutano wa pande sita utakaoandaliwa nchini China.

Baada ya mkutano wa Berlin, Korea Kaskazini ilisema ilikuwa imeafikiana kwa namna fulani na Marekani.

Mazungumzo ya pande sita yalirejewa mwezi Disemba mwaka uliopita baada ya kusitishwa kwa mwaka mmoja.

Korea Kaskazini ilitumia muda huo kufanya jaribio lake la kwanza la bomu la kinyuklia.