1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Toure ateuliwa tena kuwania tuzo ya CAF

3 Novemba 2015

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure huenda akahifadhi tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Kandanda Afrika - CAF

https://p.dw.com/p/1Gyjd
Afrikas Fußballer des Jahres 2014 Yaya Toure
Picha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Toure anayechezea Manchester City ni miongoni mwa wachezaji kumi walioorodheshwa. Aliiongoza Cote d'Ivoire na kushinda Kombe la Taifa bingwa Afrika 2015 mwezi Februrari. Ameshinda tuzo hiyo ya CAF miaka minne mfululizo tangu mwaka wa 2011. Ikiwa atafanikiwa kutwaa tuzo hiyo, atakuwa amempita Samuel Eto'o ambaye ameshinda tuzo hiyo mara nne.

Toure atapata ushindani kutoka kwa Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund ambaye anaongoza msimamo wa wafungaji bora msimu huu katika Bundesliga kufikia sasa

Mshindi ataamuliwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa na makocha au wakurugenzi wa kiufundi wa mataifa wanachama wa CAF.

Tuzo hiyo itatolewa kwenye hafla itakayoandaliwa Alhamisi, Januari 7, 2016 mjini Abuja, Nigeria.

Orodha kamili:

1. Andre Ayew (Ghana & Swansea)

2. Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)

3. Mudather Eltaib Ibrahim 'Karika' (Sudan & El Hilal)

4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

5. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)

6. Sadio Mane (Senegal & Southampton)

7. Serge Aurier (Cote d'Ivoire & Paris Saint Germain)

8. Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)

9. Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)

10. Yaya Toure (Cote d'Ivoire & Manchester City)

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu