1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Transparency International

Hamidou, Oumilkher23 Septemba 2008

Shirika linalopambana na rushwa ulimwenguni linazitaka nchi tajiri ziwe macho zaidi na kutoachia makampuni yao kuwahonga viongozi wa kigeni

https://p.dw.com/p/FNZc
Somalia iliyoteketea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe,inasemekana imezama katika bahari ya rushwaPicha: picture-alliance/ dpa


Shirika la kimataifa linalopambana na rushwa-Transparancy International limechapisha ripoti yake ya mwaka 2008 hii leo mjini Berlin.Katika ripoti hiyo Transparancy International inalinganisha rushwa katika nchi maskini kua na "janga linaloangamiza maisha ya binaadam."



Irak,Somalia,Myanmar na Haiti zinatajwa katika ripoti ya Transparancy International kua nchi ambako rushwa imekithiri.


Katika nchi masikini kabisa za dunia,rushwa inaweza kugeuka suala la uhai au mauti,mfano pale fedha za kugharimia huduma katika hospitali au za kugharimia miradi ya maji safi,zinapotumiwa vibaya" amesema hayo mwenyekiti wa shirika hilo lisilomilikiwa na serikali NGO,bibi Hugeutte Labelle wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari mjini Berlin hii leo.


Lakini hata nchi za magharibi hazijanusurika na janga hilo-ameongeza kusema.


Tangu mwaka 1995,shirika la Transparancy International limekua kila mwaka linachapisha faharasa ya viwango vya rushwa  toka jumla ya nchi 180.



Faharasa hiyo inaanzia herufi kumi kwa nchi zinazotajwa kua "zimesafika" hadi kufikia sifuri kwa zile nchi zinazotajwa kua "zimeoza kwa rushwa."


Usukani wa nchi safi unashikiliwa na Danemark,Sweeden na New-Zealand,kila moja ina faharasa ya tisaa nukta tatu,zikifuatiwa nafasi ya nne na Singapour,Finnland na Uswisi inayoshikilia nafasi ya tano .


Katika wakati ambapo rushwa inasemekana kupungua katika nchi kama vile Albania,Cyprus,Georgia,Mauricious,Nigeria,Oman,Qatar,Corea ya kusini , na Uturuki,kwengineko mfano wa Burundi au hata Uengereza Transparancy International inasema rushwa inapata nguvu.


Kuhusu Kenya,mkurugenzi wa tawi la shirika la Transparancy International nchini humo  Job Ogonda anasema:


"Kenya inajikuta katika hali mbaya sana.Yadhihriika kana kwamba rushwa ama imesalia pale pale au imezidi.Mbaya zaidi ni kwamba rushwa imeenea zaidi katika taasisi za serikali"


Transparancy International imezitolea mwito nchi tajiri zijitahidi zaidi katika kuyazuwia makampuni yao yasiwahonge viongozi wa nchi za nje na kuhakikisha kwamba benki zao zinafanya uangalifu mkubwa kuhusiana na mahala fedha zinakotokea.


"Mitindo kama hiyo inazifanya nchi tajiri zisiaminike zinapotoa miito kwa nchi masikini zipambane na rushwa" amesema mwenyekiti wa shirika la Transparancy International  bibi Huguette Labelle.


Rushwa inatishia malengo ya millenium yaliyowekwa na Umoja wa mataifa kwa nchi masikini kuweza kufikia maendeleo hadi ifikapo mwaka 2015.


Umoja wa Afrika unaashiria rushwa inaligharimu bara la Afrika dala bilioni 148 kwa mwaka,kiwango ambacho ni sawa na mapato ya ndani ya nchi tatu kwa pamoja,Kenya,Tanzania na Cameroun.


"Mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji ukaguzi wa nguvu wa mabunge,taasisi za sheria,vyombo huru vya habari na mashirika jasiri ya kijamii."Vyombo hivyo vikiwa dhaifu ,rushwa hukithiri na madhara yake kwa jamii hayakadiriki." ameshadidia bibi Labelle.


Transparancy International inataraji kwa hivyo mkutano wa wafadhili utakaoitishwa september 25 ijayo,mjini New-York,pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa utazidisha mara dufu msaada wake ili kuimarisha shughuli za taasisi hizo katika nchi masikini.