1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Libya yawatia mbaroni wahamiaji.

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3V

Maafisa wa serikali ya Libya wamesema mwezi uliopita waliwakamata watu zaidi ya elfu moja na mia moja waliojaribu kuingia Ulaya kupitia nchi hiyo.

Shirika la Habari la Libya, JANA, limesema watu wengine takriban elfu mbili waliokuwa wamekamatwa awali, walirejeshewa makwao mwezi uliopita.

Mnamo miaka ya tisini, Libya iliwaruhusu wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika kuingia kufanya kazi nchini humo kusaidia kuuinua uchumi wa nchi hiyo uliokuwa umedorora kutokana na vikwazo vya kiuchumi.

Hata hivyo serikali hiyo imeubadilisha msimamo wake siku za karibuni kwa sababu ya shinikizo kutoka mataifa ya Ulaya yayoizingatia Libya kuwa kituo kikuu cha raia wa Kiafrika wanaokimbia mataifa yao wakidhamiria kuja Ulaya kutafuta maisha.