1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Mchakato wa amani wa Darfur watathminiwa

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBid

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinasimamia mkutano wa kutathmini mchakato wa amani wenye utata kuhusu mgogoro wa jimbo la Darfur.Mkutano huo katika mji mkuu wa Libya Tripoli unatazamia kuyaleta pamoja makundi mbali mbali ya waasi na serikali ya Sudan katika kipindi cha miezi miwili ijayo.Mwaka jana ni kundi moja tu la waasi kutoka makundi makuu matatu lililotia saini mkataba wa amani pamoja na serikali ya Sudan.