1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Sudan inaunga mkono mchakato wa amani

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CE

Serikali ya Sudan imesema,ipo tayari kusitisha mapigano katika jimbo la mgogoro wa Darfur.Hayo amesema afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya mambo ya nje ya Sudan,anaehudhuria mkutano wa amani wa Darfur nchini Libya.Amesema,serikali ya Khartoum ipo tayari kusaidia mchakato wa amani kuhusu mgogoro wa Darfur.

Mkutano wa amani unaosimamiwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa umeanza leo mjini Sirte. Lakini mkutano huo umesusiwa na makundi makuu ya waasi wa Darfur na hivyo kuna shaka kama makubaliano yataweza kupatikana.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Darfur,Jan Eliasson amesema,waliokataa kuhudhuria mkutano,wanapaswa kuitumia nafasi hii kwani inawapa uwezo wa kuamua hatima ya umma wao.

Tangu mwaka 2003 makundi ya waasi katika jimbo la Darfur yanapigana na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kiasi ya watu 200,000 wameuawa na zaidi ya wakaazi milioni 2.5 wamepoteza maskani zao.