1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI : Waasi na serikali ya Chad wakubaliana juu ya amani

25 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgI

Rais wa Chad na kiongozi wa kundi moja la waasi ambalo lilijaribu kumpinduwa mapema mwaka huu wametia saini makubaliano ya amani nchini Libya hapo jana lakini waasi wangine wa Chad wametupilia mbali makubaliano hayo na kuapa kuendelea na mapambano.

Makundi kadhaa ya waasi yaliokuwa yameazimia kumpinduwa Rais Idriss Deby yamekuwa yakiendesha vita vya chini kwa chini huko jangwani,kwenye milima na porini mashariki mwa Chad na mara nyengine hata kushambulia magharibi mwa Chad.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mjini Tripoli mbele ya Rais Deby na Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kiongozi wa kijeshi wa waasi Mahamat Nour Abdelakarim amesema watu wao wameteseka na kwamba sasa lazima waharakishe usuluhishi wa kitaifa na kuleta amani nchini humo.

Makubaliano hayo yatakomesha shughuli zote za kijeshi na kampeni za kushambuliana kwenye vyombo vya habari,itawaachilia wafungwa pamoja na kutowa msamaha kwa wapiganaji kutoka pande zote mbili.