1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI: Wauguzi watano na daktari mmoja wahukumiwa kifo

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChy

Mahakama moja nchini Libya imewahukumu kifo wauguzi watatno raia wa Bulgaria na daktari mmoja raia wa Palestina kwa kuwaambukiza watoto 400 virusi vya ukimwi.

Hakimu aliyeisikiliza kesi hiyo kwa mara ya pili aliwasomea hukumu washtakiwa kwenye mahakama ya mjini Tripoli baada ya kesi kumalizika.

Washukiwa wote sita ambao wamekuwa wakizuiliwa kwa miaka saba, walikuwa wamehukumiwa kifo lakini majaji wakawapa nafasi kesi yao kusikilizwa tena kufuatia mbinyo wa kimataifa.

Kamishna wa sheria wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Franco Frattini ameshtushwa na uamuzi wa mahakama hiyo na kuitaka ifikirie hukumu yake.

Wakili wa washukiwa amesema atawasilisha malalamiko yake mahakamani.