1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tripoli yashambuliwa

Halima Nyanza(ZPR)25 Aprili 2011

Mripuko mkubwa wenye nguvu kuwahi kuukumba mji mkuu wa Libya, Tripoli kwa wiki kadhaa, umetokea mapema leo, ambao ulikuwa ukilengwa tangu kuanza kwa mashambulio makali yanayofanywa na majeshi ya kujihami ya NATO, Ijumaa.

https://p.dw.com/p/113PE
Wafuasi wa Muammar Gaddafi mjini TripoliPicha: picture-alliance/dpa

Jana Jumapili, majeshi ya serikali yaliushambulia kwa makombora mji wa Misrata, ikiwa ni siku mbili tu baada ya utawala wa nchi hiyo kusema kwamba utayaondoa majeshi yake kutoka katika mji huo unaoshikiliwa na waasi.

Ripoti zinasema watu kadhaa wameuawa.

Libysche Rebellen in der Stadt Misrata
Waasi wakikatisha katika mitaa ya mji wa MisrataPicha: AP

Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Libya, Abdelati Obeidi anaelekea katika mji mkuu wa Ethiopia, kuzungumzia mpango wa amani na Umoja wa Afrika.

Serikali ya Libya imekubali pendekezo la amani lililotolewa na umoja huo, mapema mwezi huu, lakini hata hivyo waasi wamlikataa, kutokana na kwamba halielezei kuondoka kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, madarakani.

Marekani, Uingereza na Ufaransa nazo pia zimesema hazitoacha operesheni zao za anga mpaka pale Gaddafi anaachia madaraka.