1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI:Mahakama kuamua hatma ya wauguzi na daktari wanaotuhumiwa kuwaambukiza Hiv watoto 426

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiJ

Mahakama nchini Libya inatarajiwa hii leo kuamua hatma ya waaguzi watano wakibulgaria pamoja na daktari wa kipalestina wanaotuhimiwa kwa kuwaambukiza watoto 426 virusi vya ukimwi mnamo miaka ya 1990.

Upande wa mashtaka unataka wauguzi hao pamoja na daktari wahukumiwe kifo lakini kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo huenda hilo lisifanyike ingawa haiwezi kutabirika.

Wachambuzi wa mambo wanasema uamuzi wa mahakama utachangia pakubwa katika uhusiano wa Libya na Marekani.

Waziri msaidizi wa mambo ya nje wa Marekani David Welch alifanya ziara ya siku mbili mwishoni mwa juma lililopita nchini Libya kujadili juu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na hasa juu ya kesi hiyo ya wataalamu hao wamatibabu ambao Marekani inataka waachiliwe huru.

Wataalamu hao wa matibabu wanaokanusha kufanya kitendo hicho walishtakiwa mwaka 2004 na kuhukumiwa kifo kwa kupigwa risasi lakini makahakama kuu ya Libya ikabatilisha uamuzi huo mwaka jana na kuamrisha kesi irudishwe kwenye mahakama ya mwanzo.