1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI:Mapambano ya risasi yaendelea kati ya wanajeshi na wanamgambo

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt5

Mapambano ya kufyatuliana risasi yanaendelea katika wanajeshi wa Lebanon na wanamgambo kwenye kambi ya wakimbizi wakipalestina huko Lebanon.

Mapamabano hayo yamezuka siku moja baada ya wanajeshi watano wa Lebanon kuuwawa kwenye mapambano na wanamgambo wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Al qaeda waliokwama kwenye kambi hiyo.

Duru za kiusalama zinasema wanajeshi wengine 21 walebanon wamejeruhiwa katika mapambano hayo ya risasi yaliyotokea katika kambi ya Al Bared karibu na mji wa kaskazini wa Tripoli nchini Lebanon.

Zaidi ya watu 100 wakiwemo wanajeshi 50 wameuwawa tangu kuanza kwa mapigano kati ya wanamgambo na wanajeshi wa Lebanon wiki tatu zilizopita.