1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi ataka kukutana na Kabila

9 Juni 2016

Kiongozi wa zamani wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amesema yuko tayari kwa mazungumzo na Rais Joseph Kabila. Hayo yanakuja wapinzani wanapofanya mkutano Brussels.

https://p.dw.com/p/1J3aU
Etienne Tshisekedi kiongozi wa zamani wa upinzani DRC
Picha: picture-alliance/dpa

[No title]

Upinzani umefanya "Mkutano wa Ubelgiji" wenye lengo la kushinikiza uchaguzi mkuu wa taifa lao ufanyike kama ulivyopangwa mwishoni mwa mwaka huu. Zaidi ya wajumbe 200 kutoka katika karibu vyama vyote vya upinzani nchini humo wanashiriki mkutano huo. Kutoka mjini Brussels kunakofanyika mkutano huo, DW imezungumza na mmoja wa washiriki, Mbunge Muhindo Nzangi, na kwanza anaelezea ni yapi wameyafikia mpaka muda huu.