1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tukio la mashambulizi dhidi ya watalii ni tukio la kigaidi.

26 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgI0

Nouakchot. Waendesha mashtaka nchini Mauritania wamesema kuwa wanaliangalia tukio la mauaji ya kikatili ya watalii wanne raia wa Ufaransa katika mkesha wa Chrismass kuwa ni tukio la kigaidi na kwamba majeshi ya usalama yanawatafuta watuhumiwa watatu ambao wanasemekana wanahusika na kundi la kigaidi la eneo hilo la al-Qaida. Watu watano tayari wamekwishakamatwa kuhusiana na shambulio la hapo siku ya Jumatatu karibu na mji mdogo wa Aleg na watuhumiwa wengine wanaaminika kuwa wamekimbilia katika mpaka na Senegal upande wa kusini. Mtu pekee ambaye amenusurika na shambulio hilo ambaye alijeruhiwa vibaya , amepelekwa katika hospitali kuu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.