1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya haki za bindamu na Dafur

13 Machi 2007

Halmashauri ya Haki za binadamu ulimwenguni itasikia ripoti ya tume iliochunguza kukiukwa kwa haki za binadamu mkoani Dafur,Sudan hapo alhamisi.

https://p.dw.com/p/CHIF

Licha ya mapatano ya amani yaliofikiwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita,kwa muujibu wa mabingwa wa Umoja wa Mataifa ,ukatili katika jimbo la Dafur,nchini Sudan umeongezeka.

Uhalifu wa vita na ukiukaji wa haki za binadamu umeenea kote mkoani Dafur- inasema ripoti iliotoka jana mwanzoni mwa kikao cha Tume ya Haki za binadamu ya UM.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeieralibainisha wazi mwanzoni mwa kikao cha 4 cha Tume ya Haki za binadamu ya UM mjini Geneva kuwa, Umoja wa Ulaya hautaregeza kamba na kuacha kuleta swali la kukanyagwa haki za binadamu mbele ya ajenda ya kikao hicho.Alisema,

“Umoja wa Ulaya hautaifumbia jicho hali ya mambo huko Dafur pamoja na mikasa inayoendelea ya kukanyagwa kwa haki za binadamu.Katika visa vya kukiukwa kwa haki za binadamu sisi jamii ya kimataifa, tunabeba jukumu kwa watu wa dafur la kutofumba mdomo na kujitia kitunga cha macho.”

Katika halmashauri ya haki za Binadamu mjini Geneva, nchi za kiislamu zina wingi wa kura.Hadi sasa zimekuwa zikiikinga Sudan tena na tena isilaaniwe kwa dhamana yake kwa yanayopita Dafur.

Kwa upande mwengine, nchi hizo za kiislamu zimefaulu tena mara 4 kuikashifu Israel kwa kuponda na kukiuka haki za binadamu za wapalestina.

Hata katika kikao hiki kilichoanza jana mjini Geneva,tayari kuna maazimio 3 dhidi ya Israel.

Waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Steinmeier ametoa mwito kwa halmashauri hiyo aliposema:

“Sote tunapaswa kuwa tayari kuachana na mawazo ya kuzuwia mambo kusonga mbele ikiwa tunataka kujitwika dhamana zetu na kutimiza matarajio yaliowekwa mabegani mwa halmashauri hii.

Haiwezekani kuvumilia kukanyagwa mno kwa haki za binadamu bila kuzungumzia wazi wazi kwa kuwa tu, kuna mshikamano ama wa kimkoa au wa kinadharia.

Mshikamano pekee unaostahiki kuoneshwa katika kikao hiki, ni ule wa kutetea haki za binadamu.”

Katika ripoti iliochapishwa jana kwa njia ya mtandao wajumbe wa tume ya uchunguzi ya Halmashauri ya Haki za binadamu wanaituhumu serikali ya Sudan mjini Khartoum kushiriki pia katika uhalifu katika mkoa wa Dafur.

Tume ya Haki za biandamu ikiongozwa na mshindi wa tunzo la amani la Nobel bibi Jody Williams ilikua ikague huku huko Dafur kuvunjwa huko kwa haki za binadamu .Lakini, serikali ya Khartoum ilimkatalia bibi Williams na ujumbe wake ruhusa ya kutia mguu wao Sudan.

Bibi Williams alijijuvya yapitayo Dafur kutoka kwa wakimbizi katika nchi jirani ya Chad.Bibi Williams anatazamiwa kutoa ripoti yake rasmi mbele ya Tume ya haki za binadamu mjini Geneva keshokutwa alhamisi.