1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunisia yafanya uchaguzi wa kwanza huru

Mohamed Dahman23 Oktoba 2011

Watunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza kufuatia "Uasi wa Majira ya Machipuko katika Nchi za Kiarabu"miezi tisa baada ya maandamano ya vuguvugu la umma kumn'gowa madarakani Rais Zine al- Abidine Ben Ali.

https://p.dw.com/p/RsT0
Waandamanaji wakiwa na bendera ya Tunisia wakati wa vuguvugu la umma lililompinduwa Rais Zine Ben Ali wa nchi hiyo.Picha: picture-alliance/dpa

Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza huru katika historia ya Tunisia utaweka mfano kwa nchi nyengine za Kiarabu ambapo uasi umechochea mabadiliko ya kisiasa.Tunisia ndio ilioanzisha "Vuguvugu la Majira ya Machipuko ya Nchi za Kiarabu" miezi 10 iliopita wakati maandamano ya umma kupinga umaskini,ukosefu wa ajira na ukandamizaji wa serikali yalipomlazimisha Rais Ben Ali kukimbilia Saudi Arabia. Uchaguzi wa leo ni wa baraza la katiba ambalo litarasimu katiba mpya na pia kuteua serikali ya mpito na kupanga uchaguzi wa rais na bunge nchini humo.