1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tutu ataka Zuma asichaguliwe

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cc7e

CAPE TOWN.Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama tawala nchini humo cha ANC kutomchagua Jacob Zuma kama kiongozi mpya wa chama hicho.

Amesema kuwa watu watakuwa wameiabishwa kwa Zuma kuwa kiongozi na kwamba Afrika Kusini inahitaji mtu mwengine ambaye ni bora zaidi.

Zuma ambaye mwaka jana alikabiliwa na hatia ya ubakaji lakini akashinda anawania kiti cha ukuu wa chama hicho akishindana na Rais Thabo Mbeki.

Uchaguzi wa kumchagua kiongozi wa chama hicho, utafanywa na mkutano mkuu wa ANC unaoanza kesho.

Iwapo Zuma atashinda atakuwa katika nafasi ya kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.

Akijibu shutuma za Askofu Tutu, Zuma alisema kuwa kazi ya viongozi wa wa kanisa ni kuombea watu na si kuwashutumu.

Mapema Jacob Zuma alisema kuwa iwapo atashinda kiti hicho hatobadili sera za kiuchumi za chama hicho.

Kumekuwa na shutuma kutoka kundi la mrengo wa kushoto ndani ya ANC,kwa Rais Mbeki kuwa amekuwa na sera za kuegemea zaidi upande wa biashara