1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TUTZIG : Merkel ataka Ulaya ilinde maadili ya demokrasia

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkl

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani leo ametowa wito kwa nchi za Ulaya kuchukuwa hatua ya pamoja dhidi ya magaidi wa Kiislamu na kutetea kile alichokiita maadili ya msingi ya Umoja wa Ulaya ya demokrasia na kuvumiliana.

Merkel ambaye nchi yake imeshikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya kuanzia Januari hadi mwezi wa Juni mwaka huu amewataka raia wa Umoja wa Ulaya kuona umoja huo sio tu kama chombo cha uchumi bali pia kuwa cha maadili ya pamoja.

Amesema kwake yeye kuvumiliana ni roho ya Ulaya na lazima uwe muongozo wao katika mijadala na maadui wa demokrasia na watu wa itikadi kali.

Merkel alikuwa akizungumza kwenye hotuba katika Chuo cha Avengelika cha Kanisa la Kilutheri katika mkoa wa Bavaria nchini Ujerumani.