1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tzipi Levny huenda akaongoza ujumbe wa Israel katika mazungumzo yajayo ya amani

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fq

Jerusalem

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameamua kumteuwa waziri wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni kuongoza ujumbe wa Israel katika mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati mwezi ujao nchini Marekani.Kulingana na vyombo vya habari vya Israel,waziri mkuu Olmert huenda akatangaza uamuzi huo hii leo,wakati wa mkutano wa kila wiki wa baraza lake la mawaziri.Hadi wakati huu wahariri wa kisiasa nchini Israel walikua wakiamini ,kiongozi wa pili serikalini Haim Ramon angechaguliwa kuongoza ujumbe wa Israel mazungumzoni.Kuteuliwa bibi Tzipi Livni kunaashiria msimamo mkali unaoweza kufuatwa na Israel katika mazungumzo hayo .