1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji kuunda serikali ya mpito.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdn9

Brussels. Waziri mkuu wa mpito nchini Ubelgiji Guy Verhofstadt amesema kuwa ataunda serikali ya muungano ya vyama vitano, na kufikisha mwisho wa mkwamo wa kisiasa ambao umechukua muda wa miezi sita. Nchi hiyo imekuwa bila ya serikali tangu Juni mwaka huu baada ya mkwamo wa kisiasa ambao umetishia kuligawa taifa hilo baina ya upande wa watu wanaozungumza lugha ya Kifaransa na lile linalozungumza lugha ya Kidachi. Vyama viwili vya watu wanaozungumza lugha ya Kidachi na vitatu vinavyoundwa na watu wanaozungumza Kifaransa vimekubali kuunda serikali ya muda, ambayo huenda ikaapishwa ifikapo Ijumaa wiki hii.

Wiki iliyopita maelfu ya wanachama wa vyama vya wafanyakazi waliandamana kupinga dhidi ya kushindwa kuundwa serikali na kupambana na kupanda kwa bei ya mafuta na chakula.