1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubelgiji yaombwa kumfikisha Habre mahakama ya kimataifa

9 Machi 2012

Shirika linalopigania haki za binaadam pamoja na makundi ya walioteswa nchini Chad, wameomba aliyekuwa Rais wa Chad Dikteta Hissene Habre akamatwe na apelekwe kwenye mahakama ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/14IIz
Hissene Habre
Hissene HabrePicha: picture-alliance/dpa

Maombi hayo ya kupelekwa mahakamaini yanakuja kutokana na Habre kukabiliwa na tuhuma tele, kwanza kuwatesa, kuwauwa na kuwafunga baadhi ya watu.

Ni kipindi kirefu sana tangu matukio hayo ya uhalifu yafanyike lakini kilio cha wahanga bado kipo ili haki iweze kupatikana. Huku mtuhumiwa huyo akiwa bado anaishi Senegal hadi sasa. Serikali ya Senegal ikiweka wazi kuwa haitamfungulia mashitaka yoyote yale. Wahanga hao wameamua kupeleka maombi yao huko Ubegiji ili waweze kuiomba Senegal impeleke mahakamani. Shauri hilo la maombi linasikilizwa tarehe 12 machi mwaka huu.

Habre mwenye umri wa miaka 69 yupo Senegal kwa miaka 21 sasa huku Ubelgiji ikimsaka kwa hamu na kutaka kumshitaki kwa yale aliyoyatenda akiwa madarakani. Maombi zaidi ya manne yalishatolewa kwa nia ya kupelekwa mahakmani rais huyo wa zamani lakini mara zote serikali ya Senegal imekuwa inakataa katu.

Hali hiyo imepelekea mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Askofu Desmond Tutu kuifanananisha na dhihaka kwa wale wote walitendewa maovu na Habre. Kulingana na kanuni za Umoja wa Mataifa juu ya udhalilishaji na maovu dhidi ya binadamu mtuhumiwa huyo anaweza kushitakiwa pale alipokimbilia au kurudishwa alikotokea au kushitakiwa kwenye taifa lilingine.

Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini
Askofu Desmond Tutu wa Afrika KusiniPicha: AP

Juhudi zagonga mwamba

Waziri wa mambo ya nje wa Senegal, Madické Niang kila kwa mara amekuwa akisema Habre angerudishwa Chad ambako tayari alishahukumiwa kifo kwa makosa kadhaa bila ya mwenyewe kuwepo mahakamani. Lakini hadi sasa bado hakuna jibu la kitendawili hicho .

Wakati hayo yakiendelea mwaka 2002 Serikali ya Chad ilisema ingemshitaki Habre huko Ubegiji na Chad ikaamua kumuondolea kinga ya kutokushitakiwa Dikiteta huyu ili kuweza kupekwa kizimbani huko Ubegiji.

Habre anatuhumiwa kuwafanyia maovu hata raia wa Ubelgiji ambao wao walifungua kesi mahakamani. Huku Ubelgiji mara baada ya miaka minne ya uchunguzi wa kina Jaji wa Ubegiji aliamua mwaka 2005 Habre apelekwa huko ili kuhukumiwa lakini Senegal ikaweka wazi kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa uamuzi huo.

Habre akitoka mahakamani Dakar, Senegal
Habre akitoka mahakamani Dakar, SenegalPicha: AP

Hali hii ilifanya Senegal kupeleka shauri hilo kwenye Umoja wa Afrika ambako ikaamuliwa kuwa Senegal ilishughulikie shauri hilo na Habre afunguliwe mashitaka huko huko Senegal alipo kwa niaba ya umoja wa Afrika na hili lilikubaliwa na Rais Wade lakini mpaka sasa bado hakuna kilichofanyika sababu kuu inayotolewa ni kukoseka fedha .

Serikali ya Chad mwaka 2011iliweka wazi kuwa japokuwa wahanga wengi wamefariki lakini wapo walio hai ambao wanashuhudia miongo miwili ya kuzungushwa kwa ajili ya haki yao.

Mwandishi: Adeladius Makwega

Mhariri: Hamidou Oummilkheir