1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu Ghana

7 Desemba 2008
https://p.dw.com/p/GB1p

Accra:

Uchaguzi wa rais na bunge unafanyika leo nchini Ghana. Katika uchaguzi wa rais wapiga kura watamchagua mgombea atakayechukua nafasi ya rais wa sasa John Kufour anayestaafu baada ya kumaliza vipindi viwili kwa mujibu wa katiba. Wachambuzi wanatarajia ushindani mkali kati ya mgombea wa chama cha Bw Kufour New Patriotic Party, Nana Akufo Addo na John Atta Mills wa chama cha upinzani National Democratic Congress. Vyama vyote viwili vikubwa vimeahidi utawala bora na hasa panapohusika na mapato yatakayotokana na mafuta yaliogunduliwa hivi karibuni na yatakayoanza kuchimbwa 2010. Shirika la mafuta la taifa nchini humo, linatarajia utoaji wa hadi mapipa 250.000 ya mafuta kila siku katika muda wa miaka miwili.