1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu Ghana

7 Desemba 2008

Rais Koufour amaliza muda wake.

https://p.dw.com/p/GBB1
Picha: AP

Waghana wanapiga kura leo kumchagua mrithi wa Rais John Koufour anayemaliza muda wake. Wachambuzi wanatumai uchaguzi huo utaonyesha mfano wa kuigwa katika bara la Afrika lililokumbwa na mzozo.

Katika uchaguzi wa rais wagombea wakuu wawili ni Nana Akufo Addo kutoka chama cha Bw Kufour National Patriotic Party na John Atta-Mills kutoka chama cha upinzani National Democratic Congress cha rais wa zamani Jerry Rawling.Kuna jumla ya wagombea urais saba katika uchaguzi huo-watano tangu kurudi demokrasia ya vyama vingi 1992.

Uchaguzi wa amani nchini Ghana litakua tukio la kutia moyo baada ya machafuko yaliotokea katika uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana na nchini Zimbabwe mapema mwaka huu. Mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe uliotokana na uchaguzi mkuu bado unaendelea.