1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Ethiopia

23 Mei 2010

Waethiopia leo wanapiga kura katika uchaguzi ambao Waziri Mkuu wa muda mrefu Meles Zenawi anatarajiwa kushinda.

https://p.dw.com/p/NV8P
Ethiopian Prime Minister Meles Zenawi is seen at his offices in the capital, Addis Ababa, Wednesday, Jan. 10, 2007. Zenawi said Wednesday that a U.S. airstrike in Somalia had not killed any civilians and, in his opinion, would not help create an Iraq-style insurgency or hinder efforts to build a peacekeeping force in the country. (AP Photo/Les Nauheus)
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi.Picha: AP

Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanywa Ethiopia, tangu ule wa mwaka 2005 uliogubikwa na utata na kusababisha machafuko nchini humo.

Upande wa upinzani umekiri kwamba hauna nafasi ya kuibuka na ushindi, kwa sababu, chama tawala cha "Ethiopian People's Revolutionary Demokratic Front" kimejiimarisha madarakani na mara kwa mara hutumia vitisho dhidi ya wapinzani wake na huwatia jela.

Mwaka 2005, ghasia zilienea katika mji mkuu Addis Ababa, baada ya chama tawala kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo. Wakati wa machafuko hayo, hadi waandamanaji 193 waliuwawa na vikosi vya usalama . Vile vile polisi saba walipoteza masiha yao, katika umwagaji huo wa damu uliochafua sifa ya Ethiopia,nchi inayopokea msaada mkubwa kabisa kote duniani.

Mwandishi:Munira Muhammad/RTRE

Mhariri:P.Martin