1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Ghana

11 Desemba 2008

Wananchi wa Ghana wameendelea kushikilia sifa ya utulivu na umehakikishwa tena kufuatia hofu kwamba uchaguzi uliofanyika Jumapili ungelikuwa wa ghasia kama za Kenya, Zimbabwe na hivi karibuni Nigeria.

https://p.dw.com/p/GDvZ
Wananchi wa Ghana wakiwa kwenye uchaguziPicha: AP

Ghana itafanya marudio ya uchaguzi wa rais hapo tarehe 28 mwezi wa Disemba baada ya chama tawala kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja wa zaidi ya asilimia 50.


Mohamed Dahman amezungumza na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi huru za Afrika Dr.Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa muangalizi wa Umoja wa Afrika katika uchaguzi huo na kwanza anaelezea kile cha kujifunza kutokana na uchaguzi huo wa rais na bunge ambao umeelezewa kuwa huru na wa haki.