1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Msumbiji

Sekione Kitojo31 Oktoba 2009

Rais Armando Guebuza anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais na bunge nchini Msumbuji.

https://p.dw.com/p/KJgr
Rais Armando Guebuza akipiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Msumbiji siku ya Jumatano , mjini Maputo, Oct. 28, 2009.Picha: AP

MAPUTO:

Nchini Msumbiji, Rais Armando Guebuza na chama chake cha Frelimo wanaongoza katika chaguzi za rais na bunge. Baada ya kuhesabiwa nusu ya kura zilizopigwa,Guebuza amejikingia asilimia 78 ya kura hizo na chama chake asilimia 77.

Chama cha Frelimo kilitazamiwa kushinda tangu hapo awali kwa sababu upande wa upinzani una mivutano. Hata Guebuza ametarajiwa kuchaguliwa tena. Hii itakuwa awamu yake ya pili madarakani. Chama cha Frelimo kinatawala tangu Msumbiji ilipopata uhuru wake kutoka Ureno katika mwaka 1975.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa rasmi tarehe 12 Novemba.