1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi umeanza Urusi

Sekione Kitojo4 Machi 2012

Vladmir Putin anaonekana kuwa na hakika ya kurejea tena Kremlin kutokana na uchaguzi wa rais unaofanyika nchini Urusi ,lakini atajikuta akiongoza nchi ambayo iko tayari zaidi kumpa changamoto.

https://p.dw.com/p/14Eem
epa03130617 Members of the local election commission prepare a polling station in the town of Podolsk, some 20 km south of Moscow, Russia, 03 March 2012. Russia's Interior Ministry said it had deployed around 450,000 soldiers and police to protect voters during this weekend's presidential election, Itar-Tass news agency reported on 03 March. EPA/MAXIM SHIPENKOV
Rais wa Urusi akipiga kuraPicha: picture-alliance/dpa

Wimbi kubwa la maandamano limeonyesha sehemu kubwa ya raia nchini humo wamechoshwa na hatua zinazotengenezwa na Putin za kujikita madarakani tangu alipoingia kwanza madarakani na kuwa rais mwaka 2000, na poilisi wanajiweka tayari kwa uwezekano wa ghasia za baada ya uchaguzi mjini Moscow.

Russian police officers patrol in Manezh Square in downtown Moscow, Russia, Saturday, March 3, 2012. Security is being tightened on the eve of the Russian presidential election. (Foto:Misha Japaridze/AP/dapd)
Jeshi la polisi limewekwa tayari dhidi ya ghasia za baada ya uchaguziPicha: dapd

Mfumo wa Putin wa kile kinachoitwa demokrasia yakutengenezwa, imeyaweka makundi ya kiliberali ya upande wa upinzani katika mbinyo unaoendelea , na kuwapa ruhusa ya nadra kufanya mikutano na kutuma vikosi vya polisi ambavyo vimekuwa vikivunja kwa ukandamizaji mikusanyiko ambayo haikuidhinishwa.

Serikali ya Urusi imepata udhibiti wa televisheni zote kubwa na ripoti zao za habari zimegeuka kuwa takrima ya kutokosolewa mipango ya Putin, na mara nyingi huonyeshwa picha za Putin zinazovutia akiwa amepanda farasi, akiogelea na kupiga mbizi ama akicheza na wanyama wa mwituni .

Changamoto ya maandamano

Lakini maandamano , yaliyozushwa na madai ya udanganyifu uliopindukia katika uchaguzi wa bunge mwezi Desemba , umemazimisha mabadiliko kadha.

Maafisa wametoa ruhusa , hata hivyo kwa shingo upande, kwa upinzani kufanya mikutano ambayo imekusanya watu wengi , hadi kiasi ya watu 50,000 mjini Moscow. Televisheni ya taifa imetangaza mikutano hiyo kwa kutoa maelezo yasiyopendelea upande wowote.

Iwapo uvumilivu huo utaendelea kwa upande wa serikali hilo haliko wazi bado.Kwa mujibu wa uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni , uliofanywa na shirika la uchambuzi wa maoni la kibinafsi la Levada , Putin anaelekea kushinda uchaguzi huo kwa kiasi ya theluthi mbili ya kura dhidi ya wagombea wanne, ikiwa inatosha kuweza kukanusha madai ya waandamanaji kuwa ni kundi dogo la watu wanaotumiwa.

Vibaraka wa Marekani

Putin mara kwa mara amedai kuwa waandamanaji ni vibaraka wa Marekani na mataifa ya magharibi ambao wanataka kuidhoofisha Urusi na amewatusi , kwa kusema kwa mfano kuwa nembo yao ya utepe mweupe inaonekana kama kondomu.

Russian Prime Minister and presidential candidate Vladimir Putin speaks during his meeting with his campaign activists in Moscow on Wednesday, Feb. 29, 2012. Putin warned the opposition against using illegal ways to protest the outcome of Sunday's election, in which he is all but certain to reclaim the presidency. (Foto:Maxim Shipenkov, pool/AP/dapd)
Waziri mkuu wa Urusi Vladmir Putin ambaye anawania kurejea katika kiti cha urais.Picha: AP

Katika wiki zilizopita , matamshi hayo yamekuwa makali zaidi wakati Putin aliposema hadharani kuwa upinzani uko tayari kumuua mtu wao ili kuweza kuzusha hasira dhidi yake. Madai hayo yamekuja huku kukiwa na ripoti za televisheni kuwa njama zilizopangwa na waasi wa Chechnya kumuua Putin mara baada ya uchaguzi zimezuiwa.

Mwandishi : Sekione Kitojo /ape

Mhariri: Pendo Ndovie