1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Bunge la Algeria.

17 Mei 2007

Leo unafanyika uchaguzi wa bunge la Algeria kuwachagua wabunge 389 katika uchaguzi huu wa mara ya tatu unaoendeshwa katika mfumo wa vyama vingi.

https://p.dw.com/p/CHED

Hii leo Raia wa Algeria wanapiga kura kuwachagua wabunge wepya katika Bunge la Algeria ,huku kukiweko hali ya wasiwasi kutokana na mwiito wa kundi la Al-qaeda kuwataka wananchi wa Algeria wasusie uchaguzi huo.

Karibu raia wa Algeria millioni 18.8 ndio wanaotarajiwa leo, kupiga kura kuwachagua wabunge 389 katika uchaguzi huu wa mara ya tatu wa mfumo wa vyama vingi.

Kuna vituo vya kupigia kura Elfu 42 ,wagombea wakiwa Elfu 12,229 kutoka katika vyama vya kisiasa 28

Baadhi ya watu wanasema matokeo ya uchaguzi huu huenda yasibadilishe chochote, kutokana na Rais wasasa, Abdulaziz Boutaflika mwenye umri wa miaka70 kuwa na wafasi wengi ,nawao ndio wanaotarajiwa kupata wingi wa viti.

Uchaguzi huu wa Algeria unafatiliwa kwa makini na Marekani pamoja na nchi za ulaya katika nchi hii yenye utajiri mwingi wa mafuta na gesi, Algeria ikiwa mshirika mku wa nchi za magharibi katika kupambana na waislamu wenye itikadi kali katika Mashariki ya kati.

Kwenye mkesha wakuamkia siku ya uchaguzi Askari moja wa polisi aliuwawa na watu wengine watano kujeruhiwa katika mji wa Constatine ulio watatu kwa ukubwa nchini Algeria.

Mabomu mawili ya kutengenezwa kwa mkono yaliripuka katika mkahawa moja na bomu jengine kuripuka katika kituo cha Round abaut

Hili lilikua ndio tukio kubwa kutokea tangu mwezi April mabomu matatu yaliporipuka katika mji mku Algiers na kuwauwa watu 30 na wengine 220 kujeruhiwa vibaya .

Kiongozi wa kundi la Al- Qaeda katika nchi za Afrika ya kaskazini Abu Mussaab Abdul wadud amewataka raia wa Algeria waususie uchaguzi huu

na kusema kua, yeyote atakae kwenda kupiga kura yake atakua anachangia katika uovu wa viongozi wa Algeria .

Lakini waziri wa mambo ya ndani wa Algeria Yazid Zarhouni amesema wa Algeria hawatotishwa tishwa na vitendo vya kigaidi dhidi ya mfumo wa kidemokrasia wa Algeria na amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye uchuguzi huu.

Leo ulinzi ni mkali nchini Algeria na wizara ya mambo ya ndani imeamrisha magari yote yasitembee siku ya leo, Masoko yote yafungwe na ratiba ya michezo yote iaakhirishwe.

Moja ya wangalizi wa kujitegemea katika uchaguzi huu Bi Beya Gasimi akiwa pia mwaandishi wa Jarida la lugha ya kifaransa la kila wiki, Express ,anasema uchaguzi huu utakua na mizengwe.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema ilivokua madaraka yote ya Algeria yamo mikononi mwa Rais, ambae anamaliza kipindi chake cha utawala

Mwaka 2009, raia wengi hawana imani na Bunge la Algeria ,kwahivo huenda wasijitokeze kwa wingi kupiga kura, hata ingawa leo imetolewa kuwa siku ya mapumziko nchini Algeria.