1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa bunge Urusi

2 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVjg

Mosko:

Upigaji kura unaendelea nchini Urusi baada ya vituo kufunguliwa mapema leo, kulichagua bunge jipya. ´Wakati chama cha rais Vladimir Putin”Russia ilioungana” kikitarajiwa kupata ushindi mkubwa,Vyama vya upinzani vimemshitumu kiongozi huyo kwa kutumia vibaya madaraka yake vikisema maafisa wanawabughudhi na kuwaandama wapinzani. Ushindi wa chama cha Rais Putin utamuwezesha kuwa na usemi mkubwa hata baada ya kusmaliza muda wake wa Urais mwaka ujao.

Awali kiongozi huyo alisema ushindi kwa chama chake utakua ushindi kwa rais ajaye wa Urusi.

Miongoni mwa vyama vyengine 10 vinavyogombea uchaguzi huo wa bunge ni chama cha kikoministi pekee kinachotarajiwa kupata kura zinazohitajika kuingia bungeni.