1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Georgia ulikua wa haki-inasema OSCE

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl6F

Tiflis:

Kwa mujibu wa jumuia ya usalama na ushirikiano barani Ulaya,uchaguzi wa rais nchini Georgia,umepita vizuri .Kulikua na dosari ndogo ndogo,lakini kwa jumla uchaguzi ulikua ahuru na wa kidemokrasi-wamesema hayo wawakilishi wa jumuia ya usalama na ushirikiano barani Ulaya,katika taarifa yao mjini Tiflis.Wawakilishi hao wamekosoa hasa ule mtindo wa kuchanganyishwa harakati za serikali na kampeni ya uchaguzi ya mtetezi wa kiti cha rais Michail Saakaschwili.Hata hivyo wawaakilishi wa jumuia ya OSCE wamezisuta hoja za upande wa upinzani unaodai udanganyifu umefanyika wakati wa uchaguzi.Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yanazungumzia ushindi wa rais Michail Saakaschwili kwa asili mia 60 ya kura,mpinzani wake mkubwa,Lewan GATSCHETSCHILADSE amejikingia asili mia 22 ya kura.Maelfu ya wafuasi wa upande wa upinzani wameanza kukusanyika mjini Tiflis, kupinga matokeo hayo ya uchaguzi.