1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Kenya - Rais Mwai Kibaki atangaza timu ya kampeni

27 Septemba 2007

Nchini Kenya Rais Mwai kibaki ametangaza timu yake maalum itakayomfanyia kampeni. Cha kushangaza ni kuwa viongozi vigogo hususan mawaziri wametengwa katika orodha hiyo ya watu 28.

https://p.dw.com/p/CH7b
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP Photo

Kiongozi wa taifa anapanga kuzindua rasmi kampeni ya chama cha PNU jumapili hii. Timu hiyo ilitangazwa na kundi la Kibaki tena linalosimamia kampeni za Rais kibaki kuteuliwa tena. Timu hiyo maalum inaongozwa na Rais Kibaki mwenyewe na makamu wa rais Moody Awori akiwa msaidizi wake.

Thelma Mwadzaya amezungumza na Profesa Tom Namwamba mhadhiri wa filosofia katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kuhusu tukio hilo.