1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Kenya wanukia

25 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Cg5T

NAIROBI

Kampeini za uchaguzi mkuu nchini Kenya zimekamilika ambapo wagombea wote wa kiti cha urais walifanya mikutano yao ya mwisho hapo jana katika harakati za kuwashawishi wapiga kura kuwachagua.Ghasia ziliripotiwa katika mji wa Nairobi baada ya mikutano hiyo ya kisiasa na watu kadhaa walijeruhiwa.

Kinyanganyiro cha Uchaguzi wa Alhamis tarehe 27 kinatarajiwa kuwa kigumu kati ya rais wa sasa Mwai Kibaki na mpinzani wake wa karibu Raila Odinga ambaye hadi sasa amewekwa katika nafasi nzuri ya kuweza kushinda kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo Raila Odinga katika hotuba yake ya mwisho hapo jana amerudia tena madai yake kwamba kuna njama kutoka upande wa serikali za kufanya mizengwe katika uchaguzi huo.

Baadhi ya Wagombea wengine wa kiti cha urais katika uchaguzi huo ni bwana Kalonzo Musyoka wa chama cha ODM,Pius Mwiru wa chama cha wananchi cha KPP na mwanamke pekee Nazlin Omar wa Workers Congress Party miongoni mwa wengine.