1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa mabunge ya mikoani Hesse na Niedersachsen

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyPI

WIESBADEN: Hii leo wapiga kura wanachagua mabunge mapya katika mikoa ya Hessen na Niedersachsen nchini Ujerumani.Matokeo ya uchaguzi mkoani Hesse yanangojewa kwa hamu kubwa.Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni,Waziri Mkuu Roland Koch wa chama cha CDU anaeongoza serikali ya mkoa huo tangu mwaka 1999 anakabiliana na changamoto kali kutoka mgombea wa chama cha SPD,Andrea Ypsilanti.

Kwa upande mwingine katika mkoa wa Niedersachsen,matokeo ya uchunguzi wa mwisho wa maoni yaonyesha kuwa Christian Wullf wa chama cha CDU anaeongoza serikali ya mseto pamoja na chama cha FDP ana nafasi nzuri ya kubakia madarakani.Kisichojulikana ni kama chama cha "Die Linke" kitafaulu kuingia bungeni katika mikoa hiyo miwili.Iwapo kitafanikiwa,basi itakuwa mara ya kwanza kuwakilishwa katika bunge la mikoa ya magharibi.