1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa majimbo matatu ya Ujerumani

Oumilkher Hamidou31 Agosti 2009

Awamu ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mkuu yaashiria kusisimua

https://p.dw.com/p/JM1V
Wagombea wakuu wa jimbo la Sachsen:kutoka kushoto,waziri mkuu Stanislav Tillich,mgombwa wa chama cha FDP,Holger Zastrow(kati) na Thomas Jurk wa SPDPicha: AP

Uchaguzi katika majimbo ya Sachsen,Thüringen na Saarland umewagutua wakuu wa vyama vya kisiasa mjini Berlin.Kwa namna gani matokeo ya uchaguzi huo yanaweza kuchangia kuhamasisha awamu ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi?

Pigo kubwa wamelipata katika majimbo ya Thüringen na Saarland.Katika makao makuu ya chama cha Christian Democratic-CDU, maarufu kwa jina la Konrad Adenauer-Haus-mjini Berlin wafuasi wa chama hicho cha kihafidhina walinyong'onyeya sana jana usiku."Mwangaza na kivuli"-hivyo ndivyo katibu mkuu wa chama cha CDU,Ronald Pofalla alivyotathmini matokeo ya uchaguzi huo.Kwa upande mmoja,chama cha CDU kimesalia kua nguvu kubwa ya kisiasa katika majimbo yote hayo matatu,kwa upande wa pili lakini,kinaweza kupoteza nyadhifa mbili za mawaziri wakuu-inategemea mazungumzo ya kuunda serikali za muungano yatakavyoendelea katika majimbo hayo.

Hata hivyo mkuu wa kundi la chama cha CDU bungeni,Norbert Röttgen anahisi uongozi wa kisiasa bado unadhibitiwa na chama chake.

"Ikiwa CDU hakitakua na nguvu za kutosha,basi kutakosekana uwiano bayana.Na katika enzi hizi za mizozo,Ujerumani inahitaji utulivu na uwiano bayana-hali ambayo inawezekana tuu pamoja na CDU yenye nguvu.Kimsingi huo ndio ujumbe muhimu wa kisiasa uliojitokeza leo usiku."

Katika wakati ambapo kansela Angela Merkel aliashiria hata kabla ya uchaguzi kuitishwa kwamba chaguzi za majimbo si kipimo cha uchaguzi mkuu ujao,mgombea wa kiti cha kansela kutoka chama cha SPD,waziri wa mambo ya nchi za nje Frank Walter Steinemeier anasema:

"Haya ni matokeo ya kutia moyo kwa SPD:CDU wamepoteza kura.Na kitu kimoja ni dhahir:muungano wa nyeusi na manjano(yaani muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU na waliberali wa FDP) hautakiwi humu nchini."

Deutschland Bundestag Enduring Freedom Merkel Jung und Steinmeier
Wagombea wawili wakuu wa uchaguzi mkuu ujao,kansela Angela Merkel (kulia) na Frank-Walter Steinemeier(kushoto)Picha: AP

Vyama vyote vitatu vinavyokalia viti vya upinzani katika bunge la shirikisho-Bundestag mjini Berlin,vimejikingia kura zaidi.Chama cha mrengo wa shoto Die Linke,walinzi wa mazingira Die Grüne,na waliberali wa FDP.Na wote wanajiwekea matumaini ya kufanya vizuri pia uchaguzi mkuu utakapoitishwa September 27 ijayo.Wanaojivunia ushindi mkubwa zaidi ni wafuasi wa chama cha mrengo wa shoto Die Linke.Wamegeuka kua nguzo ya pili muhimu ya kisiasa katika majimbo ya Thüringen na Sachsen na katika jimbo la Saarland wamejikingia asili mia 19 zaidi ya kura ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2004.

Mwandishi: Nina Wekhäuser/ZR/Oummilkheir Hamidou

Mhariri:M.Abdul-Rahman