1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais nchini DRC waahirishwa hadi Aprili 2019

John Juma
12 Oktoba 2017

Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahirisha uchaguzi wa rais hadi Aprili 2019. Imesema zoezi la uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Kasai ya Kati halijakamilika

https://p.dw.com/p/2lk6n
DRCONGO-POLITICS-KABILA
Picha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahirisha uchaguzi wa rais hadi Aprili 2019, ikitaja kutokamilika kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Kasai ya Kati kwa sababu ya machafuko na mapigano kati ya jeshi na waasi. Zaidi ya watu 5,000 wameuwawa  jimboni humo na zaidi ya  milioni moja kuyahama makazi yao tangu Agosti mwaka jana.

Rais wa tume ya uchaguzi amesema kucheleweshwa huko ni muhimu na kwamba maafisa watahitaji siku 504 kuandaa uchaguzi wa rais. Rais Joseph Kabila, ambaye alichukua madaraka baada ya baba yake, Laurent Desire Kabila, kuuwawa 2001, alifikia makubaliano na upinzani Desemba mwaka jana 2016 kuwa uchaguzi ufanyike Desemba 2017. Tayari Kabila amemaliza mihula yake miwili kwa mujibu wa katiba, lakini mahakama iliamuru anaweza kubakia madarakani hadi utakapofanyika uchaguzi mpya.