1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa rais waahirishwa mara ya nane Libanon

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyW

Uchaguzi wa rais nchini Libanon umeahirishwa kwa mara nyingine tena.Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa bunge,Nabih Berri imesema,uchaguzi huo utafanywa Jumatatu ijayo badala ya leo Jumanne. Hii ni mara ya nane kwa uchaguzi huo kuahirishwa nchini Lebanon.

Hapo awali,pande mbili bungeni zilishindwa kuafikiana kuhusu mtu wa kuchukua nafasi ya Rais Emile Lahoud ambae muhula wake ulimalizika mwezi uliopita.Tangu wakati huo,Libanon haina kiongozi wa taifa.Uchaguzi uliopangwa kufanywa leo hii umeahirishwa kwa sababu ya mgogoro unaohusika na utaratibu wa kubadili katiba.