1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa ubunge waahirishwa hadi Febuari 18 Pakistan

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjTT

ISLAMABAD:

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Pakistan imesema kuwa serikali inaukaribisha mchango wa jamii ya kimataifa kuhusu kifo cha kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto.

Kwa mda huohuo serikali imetangaza zawadi kwa yeyote atakaefichua washukiwa wawili ambao walionyeshwa katika picha moja wakiwa wamesimama kando mda mchache kabla ya Bi.Bhutto kuuliwa.Kifo chake ,cha wiki jana kuliidumbukiza nchi hiyo katika ghasia za kisiasa.Na mkuu wa tume ya Uchaguzi ametangaza Febuari 18 kama siku ya uchaguzi wa ubunge badala ya januari 8.Bw Qazi Mohammed Farooq amesema kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki na kuomba vyama vya upinzani kukubali matukio haya.Yeye rais Pervez Musharraf atalihutubia taifa baadae leo ambapo anatarajiwa kuomba utulivu kutanda nchini mwake.Watu wasiopungua 40 ndio wameuliwa katika ghasia zilizofutia kifo cha Benazir Bhutto.Na hayo yakiarifiwa vikosi vya Pakistan vimewauwa waislamu wenye msimamo mkali wapatao 20 katika mapigano yaliyokuwa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan. Msemaji wa jeshi la Pakistan amesema kuwa askari wanne walichukuliwa mateka hiyo jana katika eneo la milima la kusini mwa Wazirstan ambako kunapatikana wapiganaji wa Kitaliban na Al-Qaida.Katika mapigano yaliyofuatia,wapiganaji watano waliuawa papo hapo na wengine kadhaa katika mapigano mengine.Wapiganaji katika eneo hilo wanaongozwa na Baitullah Mehsud ambae analaumiwa na serikali ya Pakistan kama aliehusika na mauaji ya Benazir Bhutto yaliyotokea wiki jana.Mahsud amekanusha madai hayo.