1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa ubunge waahirishwa mwezi mmoja baadae Pakistan

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjIw

ISLAMABAD:

Wakuu wa uchaguzi nchini Pakistan wanajitayarisha kutangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge.

Matayarisho ya uchgauzi yamevurugwa na ghasia zilizotokea baada ya kuuliwa kwa kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto.Rais Perves Musharraf atalihutubia taifa leo kwa mara ya kwanza tangu Benazir Bhutto auliwe bada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Rawalpindi wiki iliopita.Licha ya wito kutoka kwa uongozi mpya wa chama cha Bi Bhutto cha Pakistan Peoples Party-PPP-na pia kutoka kwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Shariff wa uchaguzi kuendelela kama ilivyokuwa imepangwa tarehe 8 januari- lakini tume ya uchaguzi imetoa ishara kama uchaguzi wa ubunge sasa utafanyika mwezi Febuari.

Watu wasiopungua 40 ndio wameuawa katika ghasia zilizofuatia kifo cha Benazir Bhutto.