1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Ujerumani: Unakuwa vipi?

13 Juni 2017

Siku "moja" itakayoamua miaka minne ajayo. Tarehe 24 September uchaguzi wa Ujerumani utafanyika. Lakini je Ujerumani unatumia mfumo gani wa kupiga kura?

https://p.dw.com/p/2edyp
Sitzverteilung Bundestag
Viti ndani ya Bunge la UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Labda kauli muhimu na ya kila mara katika mfumo wa uchaguzi nchini Ujerumani ni:

wabunge wanachaguliwa katika " mfumo mkuu, huru, sawa na katika sehemu ya kupiga kura ya siri, yaani isio wazi."

Hivi ndivyo ilivyo katika sheria ya kawaida kifungu nambari 38, kipengele cha kwanza. Hii ina maana kuwa, watu wote kuanzia miaka 18 wanaweza kupiga kura, bila ya kujali utajiri wao, elimu au ushawishi wao katika siasa.

Kila mmoja ana kura mbili. Kura ya kwanza  ya mgombea na  nyingine kwa chama ulichokichagua. Na  chaguo la mtu ni siri, siri ya uchaguzi. Lakini mfumo wa uchaguzi wa Ujerumani ni tofauti na ule wa Marekani, Uingereza au Uswisi.

Ujerumani, muwakilishi wa demokrasia

Tofauti muhimu: Mfumo wa  kisiasa wa  Ujerumani wa utawala si wa  moja kwa moja, lakini ni ule wa uwakilishi.Uswisi  inaonekana kuwa mwakilishi  wa demokrasia ya moja kwa moja, lakini ni mfumo unaowakilisha watu. Uswisi ina  mfumo wa kipekee wa demokrasia  ambapo lkila suala zito huamuliwa kwa kura ya maoni.

Wakati nchini Ujerumani maamuzi ya kisiasa yanafanywa na wawakilishi wa watu, yaani wabunge na  hilo ndilo jukumu la kila  anayechaguliwa .

Bunge la Ujerumani : 

Tokea 2002 Bunge la Ujerumani lina jumla ya wabunge 598. Nusu ya  viti hivyo-299- huwa hazihisabiwi kwa wagombea wanaopokea kura ya wingi kwa urahisi, katika majimbo 299, kwa njia nyengine ni sawa na kusema wao huchaguliwa moja kwa moja. Zaidi ya nusu ya mamlaka ya wabunge 299  huchaguliwa kutokana na uamuzi wa wapiga kura , lakini sio kura ya moja kwa moja kwa wagombea, ila  huwa kura ya  chama katika kila kinachojulikana kama uwiano kulingan na asilimia ambayo chama husika kimepata .

KURA YA KWANZA NA YA PILI :

Kwa kila kura mbili zinapigwa na mpiga kura ni kura ya pili ndio yenye umuhimu zaidi. Hatimaye ndio yenye kuamua muundo jumla wa bunge hilo. Kwa mfano,  ikiwa chama kitapata asilimia 35 ya kura ya pili, kitawakilishwa katika bunge lijalo kwa asili  mia 35 ya viti. Na kura ya pili, mpiga kura huwa anaaamua wingi vwa wabunge.

Kipengele maalum cha sheria ya uchaguzi wa Ujerumani ni kile cha ushindi uliopatikana kwa  kufikia  kiunzi cha asilimia 5.

Wort der Woche Fünf-Prozent-Hürde
Picha inayoonyesha kiunzi cha asiliamia 5 cha kuweza kuingia katika bunge Picha: DW

Katika nchi nyingine pia,kuna mahitaji ya kiwango cha asilimia ya kura  kuweza kuingia bungeni ; Nchini Israeli ni asilimia 3.5  na asilimia 10  Uturuki. Ujerumani, asilimia 5 ndio kigezo cha kuwa na uwakilishi katika bunge.

Mwandishi: Najma Said

Mhariri: Mohamed Abdul Rahman