1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Ukraine magazetini

29 Oktoba 2012

Mada tofauti zimechambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo,kuanzia mgogoro wa fedha nchini Ugiriki,bajeti ya mwaka 2013 ya Ujerumani,hali nchini Syria,Uchaguzi wa Ukraine na kadhalika.

https://p.dw.com/p/16Yj1
Klaus Masuch,mwakilishi wa benki kuu ya Ulaya,mmojawapo wa wawakilishi watatu-wafadhili wa UgirikiPicha: Angelos Tzortzinis/AFP/GettyImages

Tuanze lakini na ripoti ya pande tatu-yaani Benki kuu ya Ulaya,shirika la fedha la kimataifa na Umoja wa ulaya kuhusu msaada ziada kwa Ugiriki.Gazeti la "Ludwigsburger Kreiszeitung" linaandika:

Huenda ripoti ya wataalam wa pande hizo tatu imekawia kuchapishwa kwasababu waasisi hawajaweza kukubaliana hatua kali za aina gani za kufunga mkaja wanataka Athens ifuate ili iweze kupatiwa misaada ziada ya fedha.Ukweli lakini ni kwamba safari hii walipa kodi hawatosalimika.Kwasababu,vyovyote vile watalaam wa kundi la pande tatu watakavyopendekeza,fedha za walipa kodi zitahitajika.Na kenda haiko mbali na kumi.Ukweli utajulikana tu.Athens itahitaji mkopo mwengine kuanzia mwezi ujao wa November.Jinsi wanasiasa wanavyojaribu kulikwepa suala hili,inamfanya mtu akumbuke lile suala kama watu wajiandae kabisa kwa msimu wa baridi, msimu wa mapukutiko unapowadia na jibu likawa:Ah,tusubiri kwanza!

Ukraine Wahl Stimmen Stimmenauszählung Kiev
Kura za uchaguzi wa bunge la Ukraine zahesabiwa mjini KievPicha: Reuters

Uchaguzi nchini Ukraine pia umehanikiza magazetini hii leo.Na gazeti la "Neue Osnabrücker Zeitung" linaandika:'

Ukraine inaelekea wapi?Makadirio ya kwanza baada ya uchaguzi wa bunge,hayaashirii mema:Yanaonyesha nchi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya,haielekei magharibi na katika Umoja wa Ulaya.Kama itaijiongelea zaidi Urusi,hali hiyo itabainika miezi ijayo.Chama tawala cha rais Viktor Yanukowitsch,rafiki mkubwa wa ikulu ya Urusi-Kreml kinaonyesha kuongoza na kitaendelea kutawala pamoja na wakoministi.Hilo ni pigo kubwa kwa upande wa upinzani.Nchi hiyo na wakaazi wake milioni 45 bado imegawanyika-sehemu ya magharibi inapendelea kujiunga na Umoja wa ulaya na sehemu ya mashariki wanakoishi watu wanaozungumza kirusi wanaiangalia Urusi kuwa ndie mshirika wao.Mtu mshupavu kama Yanukovitsch sie kiongozi anaefaa kuwaunganisha wananchi wa Ukraine.Kwa bahati mbaya:

Syrien Kämpfe Aleppo 28.10.2012 Rebell
Mapigano yapamba moto AllepoPicha: Getty Images

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamemulika pia hali nchini Syria baada ya maridhiano ya kuweka chini silaha katika kipindi cha Idd El Adha.Gazeti la "Heilbronner Stimme" linaandika:

Mjumbe wa kimataifa Lakhdar Brahimi ana kazi kubwa.Juhudi zote za kuleta amani tangu zile za wapatanishi wa nchi za kiarabu mpaka zile za Kofi Annan zimeshindwa .Pande zinazohasimiana zimesimama kwa shari dhidi ya upande wa pili.Fursa pekee aliyokuwa nayo Brahimi, ingawa ni dhaifu,ilikuwa siku kuu ya Idd Al Adha ambapo pande zote zinazopigana vita zilikubali kusitisha mapigano.Lakini fursa hiyo haikutosha kujenga msingi imara wa kuweka chini silaha.

Deutschland Finanzminister Wolfgang Schäuble in Berlin
Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang SchäublePicha: dapd

Na mada yetu ya mwisho magazetini hii leo inahusu bajeti ya mwaka 2013 nchini Ujerumani.Gazeti la "Kieler Nachrichten" linaandika:

Pindi serikali ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na waliberali wa FDP,ikifanikiwa kweli kusawazisha bajeti ya mwaka 2013,baasi bila ya shaka yoyote,tukio hilo litakuwa na umuhimu mkubwa.Tangu mwaka 1962,serikali zote zilizoingia madarakani zimekuwa zikitumia fedha nyingi zaidi ya zile inazopata.Fursa hii mpya si matokeo ya hatua za kijasiri za kupunguza ruzuku na kujizuwia katika sera za kugharimia miradi tofauti.Ni jaza ya hali isiyo ya kawaida ya ukuaji wa kiuchumi ikichanganyika na utaratibu usio sawa wa kodi za mapato ulioifanya serikali kujikingia mabilioni ya fedha.

Mwandishi;Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman