1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wakhairishwa tena

29 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Chsv

BEIRUT

Uchaguzi war ais nchini Lebanon uliotazamiwa kufanyika leo umekharishwa kwa mara nyingine tena.Spika wa Bunge nchini humo Nabih Berri amesema uchaguzi huo utafanyika katika kikao kingine cha bunge cha mwezi januari 12.Hii ni mara ya 11 kwa uchaguzi huo kukhairishwa kufuatia mivutano ya kisiasa inayoendelea nchini humo. Kiti cha rais kimekuwa wazi tangu pale rais Emile Lahoud alipomaliza kipindi chake madarakani mnamo tarehe 23 mwezi Novemba.Muungano unaoungwa mkono na nchi za Magharibi na kundi la upinzani likiongozwa na Hezbollah walikubaliana kwamba generali mkuu wa majeshi Michel Suleiman achukue nafasi hiyo lakini mzizi wa fitna uliobakia ni juu ya kugawana madaraka katika serikali mpya itakayoundwa pindi Suleiman atakuwa rais wa nchi hiyo.