1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi wa wahariri

3 Aprili 2007

Safu za wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani ziliegemea zaidi mada 2:Kwanza mkutano wa jana wa kilele juu ya ulezi wa watoto wadogo kabisa ili wazee waweze kufanya kazi.Mada ya pili ni kutumika kwa ndege za kivita za Ujerumani "Tornado" nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/CHTL

Katika hicho kilichoitwa “mkutano wa kilele wa nafasi za ulezi kwa watoto wadogo”, tangu waakilishi wa serikali za mikoa hata wale wa za wilaya waliungamkonokuwa idadi ya nafasi za ulezi ziongezwe mara tatu hadi ifikapo 2013 nazifikie jumla ya 750.000.

Swali sasa ni jinsi gani kugharimia mradi huo.Kwahivyo, katika shina la uchambuzi wa wahariri mada ya familia imeibuka safu ya mbele kabisa katika sera za ndani za Ujerumani.

Kwa mfano, gazeti la GENERAL ANZEIGER linalotoka hapa Bonn linaandika:

“Ikiwa siasa na watungaji siasa hizo zinahusu moja kwa moja maisha ya wanadamu,huo ni mwanzo mwema.Na hii ni sawa na uamuzi wa jana ulioamua kuwa hadi ifikapo 2013 nchini Ujerumani alao kwa kila motto watatu kuna nafasi katika kindergarten.

Haja ya kuwa na nafasi kama hizo ni kubwa mno.Kwani wazee wengi-mke na mume wanataka au wangependa au walazimika kufanya kazi.Kwahivyo, inafahamika akina mama wengi vijana hufikiria kuwa waja wazito,endapo kazi na ulezi wa watoto unafungamana pamoja.”

FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Frankfurt, linaelezea shaka shaka zake hapo linaposhindwa kuelewa kwanini kuna paparapara nyingi hapa!

“Kila kitu sasa kitekelezwe harakay.Wazee wenye watoto wadogo hawamudu tena kungoja.Waziri wa familia anawaharakisha wanasiasa tangu wale wa shirikisho hata wa mikoa kuchukua hatua.

Kwa mtindo huo wa kuharakisha mambo yatendeke sasa hivi,Bibi von der Leyen,alifaulu kupitisha mradi wake wa malipo ya wazee.Sasa anatumia mtindo huo huo kupitisha mradi wake wa kuongeza mara 3 nafasi za ulezi wa watoto katika kindergarten.

Swali jinsi gani kuugharimia mradi hu na nani atachukua gharama hizo limepewa kitambo kisogo kana kwamba si muhimu.”

Hebu tusikie sasa maoni ya ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz likituhetimishia mada hii.Linaonya kuwa katika mjadala huu wote, hatima ya watoto wenyewe isifumbiwe macho:Laandika:

“Shabaha hapa sio tu iwapo bali vipi ulezi huu wa watoto unafanyika.Kwani, jamii inayotamani watoto zaidi,yapaswa kuthibitisha kuwa kweli inawatakia kweli heri na mema.

Katika kufanya hivyo ni kuzingatia sifa za malezi,idadi ya walezi wanaowahudumia watoto hao,sifa zao,ushirikiano wao na wazee na halkadhalika, swali la fedha.Maswsali haya yote muhimu hivi sasa hyayatiwi maanani.”

Gazeti la LÜBECKER NACHRICHTEN linatuchukua sasa katika medani ya vita huko Afghanistan na uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka huko ndege zake za kivita chapa “Tornado”.

“Ujerumani tayari sasa iko vitani.Ikiwa ilichelewa, basini baada ya kuanza kutumika ndege zake za Tornado.Si muhimu, iwapo ndege hizo zinashiriki moja kwa moja katika mapigano au kama nchini Bosnia, zinapiga doria tu kutambulisha wapi walipo maadui.

Kwani, yule ambaye kwa njia hii anaziba pengo la udhaifu wa NATO kama asemavyo waziri wa ulinzi Bw.Jung,huyo ni mshirika vitani.Kukanusha hayo, ni sawa na kujitia kitunga cha macho.”

ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz lina hisi :

“ yote ni sawa iwapo marubani wa kikosi cha Bundeswehr na ndege zao wanafanikiwa huko Afghanistan au la,Ujerumani kwa kupeleka ndege hizo, imejiunga na kundi la nchi zinazoshiriki vitani na haiwezi tena kujidai shughuli zake ni ujenzi mpya wa Afghanistan na kusimamia ulinzi.Na hii itakuwa na athari zake kwa wanajeshi wote wa Ujerumani walioko huko.”

OFFENBACH-POST linachambua:

“Haiwezekani kabisa kuwa mara tu zikiwasili ndege hizo Afghanistan,zitaweza kuondoshwa majira ya kiangazi pale muda wa jukumu la Ujerumani huko ukimalzika…..

Lakini, serikali ya Ujerumani yatoa dhana kana kwamba, jukumu lake huko, ni kujilinda tu na hatari linaloikabili yaweza kukisiwa-la hasha-sivyo kabisa.”