1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

240110 Wirtschaft Ethik

Sekione Kitojo25 Januari 2010

Jukwaa la kiuchumi duniani, linalofanyika mjini Davos, na mkutano wa kijamii unaofanyika Porto Alegre haya ni matukio makubwa yanayopingana.

https://p.dw.com/p/LgBk
Jukwaa la kiuchumi duniani mjini Davos katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban, rais wa Nigeria Yar'Adua, waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.Picha: picture-alliance/ dpa

Jukwaa la kiuchumi duniani, linalofanyika kila mwaka mjini Davos, na mkutano wa kijamii unaofanyika mjini Porto Alegre, mtu anaweza kusema kuwa ni matukio makubwa yanayopingana. Baadhi ya masuala muhimu, hata hivyo, yanakubaliana. Vipi uchumi katika karne hii ya 21 uendeshwe. Vipi mataifa yanaweza kutoa uamuzi katika mikutano ya kimataifa. Na hususan , ni maadili gani sisi kama binadamu yanaweza kutuongoza katika karne hii mpya.

Mjini Davos viongozi wa makampuni na masoko ya hisa kwa muda wa miaka 40 yamekuwa yakihudhuria mkutano huo unaojulikana kama jukwaa la kiuchumi, ambapo hadi sasa mialiko imekuwa ikitolewa na jukwaa hilo. Nchini Brazil, katika mji wa Porto Alegre, katika jukwaa la mkutano wa kijamii kila mtu anakaribishwa, na katika mkusanyiko huo kuna mengi ya kubadilishana kuhusiana na masuala ya kisheria na kijamii duniani.

Kwa mtazamo wa haraka, wakati malengo ya mkutano wa kijamii unaofanyika Porto Alegre na jukwaa la kiuchumi la dunia mjini Davos hayafanani , mada zao zinafanana. Ikiwa ni mkutano unaopingana na lengo la utandawazi duniani, washiriki wa mkutano huo wamekubaliana , kwamba utandawazi hauwezi tena kuzuiwa , badala yake unaweza tu kuridhiwa. Na kwa upande wa jukwaa la kiuchumi la Davos , muasisi na kiongozi wa jukwaa hilo Klaus Schwab, amekiri kuwa utandawazi sio tu suala la kiuchumi pekee.

Ni kweli kwamba tunakabiliwa hii leo na dunia iliyo pamoja, ikiwa na maana kuwa matatizo yetu yatuhusu wote na hii ina maana kuwa tunapaswa kutafuta njia ya kufanyakazi kwa pamoja kama jamii ya dunia. Nikiangalia miaka 40 iliyopita maslahi yalikuwa juu ya taasisi za kitaifa, na makampuni , lakini hii leo Davos ni sehemu ambapo tunaiangalia dunia kwa jumla.

Kama anavyosema Corman Cullinan, mmoja wa viongozi wa kundi la ulinzi wa mazingira duniani , kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukiangalia sehemu moja tu, ambapo kipimo cha maadili pia kinahitajika kuhusiana na uchumi.

Tatizo kuu ni kwamba tumekuwa tuking'ang'ania mambo ya kifikra tu, kwamba tunahitaji tuna udhibiti kamili wa sayari yetu na kwamba udhibiti huo ni mzuri. Tunapaswa kujitenga na fikra hizo. Ikiwa mahitaji yetu yanaongezeka kila siku, hatutatosheka. Hata kama zitakuwapo sayari 50 kama dunia hazitatosha, kwasababu tunahitaji zaidi na zaidi.

Haya ni masuala ambayo sio tu yanapaswa kujadiliwa katika majukwaa ya kiuchumi huko Davos na Porto Alegre pekee badala yake ni suala la kujadiliwa na dunia nzima.