1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa Ujerumani katika mwaka wa uchaguzi

16 Juni 2017

Kwa mtazamo wa kwanza, kila kitu kiko sawa, ukuaji wa uchumi wa Ujerumani unaonyesha kuwa imara ukiwa na asilimia 1.9 mwaka 2016 na ukosefu wa ajira ni kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miongo kadhaa.

https://p.dw.com/p/2eg9Y
Symbolbild USA Hafen von Charleston
Picha: Picture alliance/R. Cummins/robertharding

Hata makampuni yana matumaini na bidhaa zao kuanzia makampuni ya magari yale ya kuuza vifaa vya mashine hadi makampuni ya madawa; biashara zao za kuuza nje zimeimarika. Uchumi kwa hivyo unakwenda bila mashaka.

Pamoja na uchumi kuonekana kuboreshwa, kuna wengine wana wenye hofu.Yapo maeneo ambako kuna hali mbaya ya barabara, madaraja na hata shule.

"Hii ndio mojawapo ya sura mbaya ya Ujerumani," inasema ripoti ya mwisho ya Tume  ya Wataalamu, ambayo ilichunguza hali ya miundombinu ya umma kwa niaba ya Wizara ya Uchumi tangu 2014.

Kuna msongamano wa magari zaidi 1,900 kwa siku Ujerumani, kwa mujibu wa Chama cha Vyombo vya Usafiri (ADCA). Hakuna siku Ujerumani iliyokuwa matreni hayachelewi na kutokuwa na matatizo. Katika kila watoto kumi ambao wazazi wao wana haki ya kimsingi ya kulelewa, mtoto mmoja hapati nafasi hiyo katika shule za chekechea.

Japo kuwa watu wamechukua hatua za kisheria. Na mabwawa ya kuogelea 1041 yamefungwa au yako katika harakati za kufungwa.

Alternativen zur Silvesterparty
Treni nchini Ujerumani katika kituo kimoja mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

"Matumizi ya umma yamepungua, huduma nyingi za umma pia zimeporomoka au zimegeuzwa kuwa huduma za watu binafsi. Malipo yameongezwa na malipo ya vitu vengine ambayo yalikuwa hayapo awali sasa yapo," limelalamika shirika la chama cha wafanya kazi katika ripoti ya wataalamu wa tume hiyo.

Bajeti kidogo katika mfumo wa elimu:

Pia Ujerumani inawekeza pesa kidogo katika mipango ya elimu kulinganishwa na nchi za OECD, ambazo ni nchi 25 za kitajiri. Nchi hizi  zinatumia asilimia 5.2 kutoka mfuko wao wa uchumi kwa ajili ya elimu. Lakini Ujerumani inatumia asilimia 4.3 tu.

Deutschland Flüchtlingskinder in Grundschule in Frankfurt an der Oder
Shule nchini UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/P. Pleul

Hivi karibuni Ujerumani imekuwa ikiachwa nyuma katika masuala ya elimu, na kushindwa kushikilia nafasi kumi za mwanzo.

Wengi wameweza kufurahia kuongezeka kwa mapato ya kawaida, ambayo yamepanda kwa asilimia 2 katika kipindi cha miaka mitatu.

Tabaka la kati la wajerumani wana wasiwasi kwasababu limekuwa likinyweya kwa kipindi cha miaka 30 kwa mujibu wa kituo cha mapato na wachunguzi wa chuo cha kazi, cha chuo kikuu cha Duisburg Essen. Wakati huo huo idadi ya wale wenye mapato madogo au wale wanaopata mapato makubwa idadi yao pia inazidi kupanda. Kwa jumla utafiti huu unaonesha kutokuwepo kwa usawa katika usambazaji wa mapato, kutokana na wachunguzi hao.

Ujerumani ina moja ya sekta kubwa ya mshahara wa chini katika nchi za  Umoja wa Ulaya- ikiwa na asilimia 23 wafanyakazi  wenye kipato cha  mshahara mdogo. Katika nchi kama vile Italia, Ufaransa, Denmark na Finland,ni  chini ya asilimia kumi, Ubelgiji na Sweden, ni chini ya asilimia tano.

Na hatimaye, takwimu za ukosefu wa ajira ni sehemu tu ya ukweli. Ukweli ni kuwa katika mwezi wa Mei 2017, chini ya watu milioni 2.5 walikuwa bila kazi, ambacho ilikuwa kiwango cha chini kabisa tangu mwaka 1991. Lakini jumla ya watu milioni 6.2 wanategemea msaada wa serikali. Watu hawa wanajumuisha wale wasiopata kipato cha kutosha kumudu kuishi, wakiwemo watoto katika familia hizi.  Kiwango cha watu wanaotegemea msaada wa kijamii hakijashuka tokea tangu mageuzi makubwa yaliotokea kati ya mwaka wa 2005 na 2010.

Kuna maswali mengi ya kiuchumi mwaka huu: Lazima serikali sasa iwekeze zaidi katika miundombinu na elimu? Au lazima uchumi ushuke tena? Lazima, kukata kodi ili wananchi wawe na  fedha zaidi katika mifuko yao? Na vipi kuhusu haki za kijamii kitu ambacho chama cha  SPD kimechagua kuwa  ndio kauli ya kampeni yake ya uchaguzi?

Masuala yote haya yanazua  utata. Pia kuna suala la matumizi ya wakimbizi na wahamiaji kwenye gharama kutoka nishati  hadi dhamana ya ulaya  na kuwepo kwa uwezekano wa kuyakata  madeni ya Ugiriki.


Mwandishi: Najma Said
Mhariri: Saumu Yusuf